• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Patriots ndiyo mabingwa wa ligi kuu msimu wa 2017/2018

    (GMT+08:00) 2018-05-07 10:10:18

    Timu ya Patriots ndiyo mabingwa wapya wa ligi ya kikapu nchini Rwanda kwa msimu wa mwaka 2017/2018, licha ya kuwa katika mechi yao ya mwisho walifungwa na wapinzani wao REG.

    Ubingwa huu inakuwa ni mara ya pili mfululizo kwa Patriots baada ya kuwa walifanya hivyo tena msimu wa mwaka jana.

    Pamoja na zawadi ya kombe la ubingwa, Patriots wa walikabidhiwa fedha taslimu, faranga za Rwanda milioni 1.5.

    Katika mechi yao ya mwisho, Patriots walifungwa kwa alama 57-64 na REG ambao sasa ndiyo walishinda nafasi ya pili na kujizolea zawadi ya fedha faranga za Rwanda milioni 1.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako