• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Viwanda viwili vipya kuanza kuzalisha saruji Tororo

    (GMT+08:00) 2018-05-08 17:16:32

    Viwanda viwili vipya vitaanza hivi karibuni kuzalisha saruji katika wilaya ya Tororo nchini Uganda.

    Viwanda hivyo ni vya kampuni za Simba Cement na Hima Cement na vinatarajiwa kupunguza bei ya bidhaa hiyo,

    Simba na Hima Cement vitafungua viwanda hivyo katika vijiji vya Tutir na Nyakesi katika barabara ya Tororo-Mbale.

    Viwanda hivyo vinatarajiwa kufungua nafasi 2,500 za ajira na kuongeza uzalishaji wa jumla wa bidhaa hiyo nchini Uganda.

    Maneja wa Simba Cement, nchini Uganda Vishnu Patel, amesema kiwanda hicho kinalenga kuzalisha tani 3,000 za saruji kwa mwaka na kuajiri watu 200 moja kwa moja.

    Naye mkurungez wa Hima cement Nicholas George, amesema wataajiri zaidi ya watu 250.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako