• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: GroFin na wakfu wa Mastercard kuanza kusaidia biashara ndogo ndogo Rwanda

    (GMT+08:00) 2018-05-08 17:17:04

    Taasisi ya kibinafsi ya kifedha nchini Rwanda GroFin imeshirikiana na wakfu wa Mastercard kuanza kusaidia biashara ndogo ndogo na wajasiriamali katika sekta ya utalii kupitia kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha na kujenga uwezo.

    Mpango huo wa Mastercard wa miaka mitano kwa jina Hanga Ahazaza unatarajiwa kupunguza umaskini kwa kuongeza nafasi za ajira kwa vijana.

    Mpango huo wa dola milioni 50 unaendana na mtazamo wa GroFin wa kuongeza nafasi za ajira kwa vijana na wanawake.

    Hanga Ahazaza, ambayo inamaanisha 'kujenga siku za usoni' itawapa vijana na wanawake 30,000 ujuzi wanaohitaji kabla ya kuingia kwa ajira na kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha na ujuzi wa kuendeleza biashara ndogo ndogo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako