• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • EAC: EAC kuunganisha viwango vya ukaguzi wa magari

    (GMT+08:00) 2018-05-08 17:17:54

    Nchi za Jumuiya za Afrika Mashariki (EAC) zinapanga kuunganisha viwango vya ukaguzi wa magari ili kuongeza usalama wa barabarani.

    Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Magari katika Mamlaka ya Taifa ya Usafiri na Usalama (NTSA) NCHINI Kenya Gerald Wangai, amesema kwamba sasa kila mmoja wa nchi sita za EAC ina viwango tofauti vya ukaguzi wa magari.

    Amesema wakala wote wa usalama wa barabara katika EAC wamekubali kupitisha kiwango kimoja cha ukaguzi wa magari ili kuhakikisha ajali zimepunguzwa.

    Wangai alisema kuwa usawa wa viwango vya ukaguzi wa gari utawezesha kutambuliwa kwa pamoja kwa vyeti vya kitaifa vya ukaguzi na nchi nyingine wanachama.

    Aliongeza kuwa kutokana na viwango tofauti vya magari ya kitaifa, wamiliki wa magari wanalazimika kupitia ukaguzi na nchi nyingine za wanachama wa EAC na hivyo kupoteza muda mipakani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako