• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Ushuru wa mafuta kuongezwa Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-05-08 17:19:00

    Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji nchini Tanzania imeitaka Serikali itekeleze ushauri wake na agizo la Bunge la kuongeza tozo kwenye mauzo ya dizeli na petroli kutoka shilingi 50/- hadi Sh 100/- kwenye kila lita ili kutunisha Mfuko wa Maji.

    Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mahmoud Mgimwa, kutotekelezwa kwa ushauri na agizo hilo kumeathiri maendeleo ya sekta ya maji.

    Ameyasema hayo wakati anatoa maoni ya kamati kuhusu utekelezaji wa bajet ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa mwaka wa fedha 2107/2018 na makadiriio ya mapato na matumiz ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2018/2019.

    Amesema, kutoongeza tozo hizo kumeathiri ufanisi wa Mfuko wa Maji ikiwa ni pamoja na kukwamisha utekelezaji wa miradi ya maji hasa vijijini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako