• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China kutangaza bidhaa za uvumbuzi wa kiutamaduni ng'ambo

  (GMT+08:00) 2018-05-08 17:58:46

  China itaandaa Maonesho ya Bidhaa za Uvumbuzi wa Kiutamaduni katika sehemu mbalimbali duniani, ili kutangaza bidhaa hizo. Maonyesho hayo ni sehemu ya juhudi za China kufahamisha utamaduni wake kwa nchi nyingine duniani.

  Naibu mkurugenzi wa idara ya mawasiliano na nje ya wizara ya utamaduni na utalii ya China Bw. Zheng Hao, amesema kuanzia Mei 10 hadi Juni 30, China itafanya Maonesho ya Bidhaa za Uvumbuzi wa Kiutamaduni ya China kwenye vituo vya utamaduni wa China vilivyopo katika sehemu mbalimbali duniani, ili kutangaza bidhaa hizo kwa wageni. Anasema,

  "Tutaandaa shughuli 86 kwenye Maonesho ya Bidhaa za Uvumbuzi wa Kiutamaduni ya China, ambazo zinahusiana na sekta za majumba ya makumbusho, utamaduni usioonekana, ubunifu, katuni na teknolojia za kidigitali. Bidhaa hizo ni pamoja na zile zilizobuniwa na mashirika yanayomilikiwa na wizara ya utamaduni na utalii na bidhaa zilizobuniwa na majumba ya makumbusho, mashirika ya ubunifu na mashirika ya uvumbuzi wa kiutamaduni."

  Bidhaa nyingi zinazobuniwa na mashirika mbalimbali likiwemo jumba la makumbusho la kasri la mfalme, shirika la stempu la China CNPC zinapendwa na watu nchini China. Mkuu wa miradi wa Shirika la CNPC Bw. Tang Jing amesema, watawafahamisha watazamaji wa kigeni utamaduni wa jadi wa China na utamaduni wa nchi za "Ukanda Mmoja na Njia Moja". Anasema,

  ""Tumechagua stempu za mashairi 300 za enzi ya Tang ambazo maandishi elfu 25 ya kichina yamechapishwa kwenye stempu hizo. tumeandaa kifaa cha kusomea mashairi hayo, ili kuonesha stempu hizo,. "

  Kituo cha mawasiliano ya utamaduni kati China na nchi za nje kinataka kupeleka bidhaa za aina 800 hivi za utamaduni wa China kote duniani. Mkuu wa miradi wa kituo hicho Bw. Li Yu amesema, watakachoonesha ni pamoja na maandishi ya kichina, mandhari safi ya Dunhuang, na maajabu ya Kungfu. Anasema,

  "Kwa sababu marafiki wa Afrika wanapenda sana Kungfu, hivyo tutaonesha bidhaa zinazohusiana na hekalu la Shaolin nchini Benin na Mauritius. Mbali na hayo, tutatumia teknolojia ya VR kuwasaidia watazamaji kupata video ya kujifunza mazoezi ya viungo ya jadi ya China yanayoitwa Baduanjin."

  Imefahamika kuwa vituo vya utamaduni wa China vilivyopo katika nchi 29 vitashiriki kwenye shughuli husika za Maonesho ya Bidhaa za Uvumbuzi wa Kiutamaduni ya China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako