• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kongamano la tatu la Baraza la Ushirikiano wa Serikali za Mitaa za China na Afrika lafanyika hapa Beijing

    (GMT+08:00) 2018-05-08 20:31:00

    Kongamano la tatu la Baraza la Ushirikiano wa Serikali za Mitaa za China na Afrika limefanyika hapa Beijing, na kuhudhuriwa na viongozi kutoka China na nchi nyingine wakiwemo Makamu wa rais wa China Bw. Wang Qishan, Waziri mkuu wa Niger Bw. Brigi Rafini, waziri mkuu wa zamani wa Tanzania Bw. Salim Ahmed Salim.

    Bw. Wang amesema, ujamaa wenye umaalum wa kichina umeingia katika zama mpya, na China imekumbatia mabadiliko makubwa ya kuwa na nguvu zaidi. Amesema China itaendelea kutekeleza sera ya kufungua mlango wazi na kunufaishana. Anasema,

    "China na Afrika siku zote zinasaidiana na kuungana mikono. China inapenda kutumia maendeleo yake kuhimiza maendeleo ya Afrika. Chini ya utaratibu wa FOCAC, serikali za mitaa za pande mbili zinafuatilia ushirikiano na mawasiliano ya "Kuondoa Umaskini na Maendeleo Endelevu", ambayo yatasaidia kuhimiza kuweka mzizi wa uhusiano wa ushirikiano wa kiwenzi na kimkakati wa pande zote kati ya China."

    Mkuu wa mkoa wa Turkana nchini Kenya Bw. Josphat Koli Nanok amesema, kuondoa umaskini ni changamoto ya pamoja inayozikabili nchi zinazoendelea, na ushirikiano kati ya serikali za mitaa unaendana na sera za kurahisisha sera na kuzipatia serikali za mitaa mamlaka nyingi zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako