• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Bei ya gesi kwa maskini yapungunzwa Kenya

    (GMT+08:00) 2018-05-08 20:59:47

    Wizara ya fedha nchini Kenya imetoa shilingi bilioni 2 za kusaidia kupunguzwa bei ya gesi kwa familia masikini.

    Sasa mtungi mmoja wa gesi kilo sita na meko zitauzwa kwa shilingi 2,000 badala ya elfu 5,000.

    Kutolewa kwa fedha hizo ni mpango wa serikali wa kupunguza utegemeaji wa makaa na mafuta taa kwa shughuli za upishi.

    Mitungi ya gesi kwa jina Gas Yetu, itasambazwa kwa familia maskini kupitia kampuni ya kuuza mafuta ya National Oil.

    Chini ya mpango huo ambao umefanyiwa majaribio katika kaunti za Machakos na Kajiado wizara ya kawi inapanga kununua na kusambaza mitungi milioni 1 ya gesi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako