• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yarusha satelaiti mpya ya uchunguzi wa mazingira

    (GMT+08:00) 2018-05-09 10:12:48

    China imerusha satelaiti Gaofen-5 ya uchunguzi wa mazingira ambayo ni sehemu ya mradi wa taifa wa uchunguzi wa dunia.

    Satelaiti ya Gaofen-5 imerushwa leo alfajili kwa kutumia roketi ya Long March 4C kutoka kwenye Kituo cha kurushia satelaiti ya Taiyuan mkoani Shanxi, China. Hii ni mara ya 274 kwa roketi ya Long March kutumika.

    Msanifu mkuu wa satelaiti hiyo Bw. Tong Xudong amesema satelaiti ya Gaofen-5 ni ya kwanza iliyotengenezwa na China inayoweza kusimamia uchafuzi wa hewa na utoaji wa gesi ya kaboni, na pia ni ya kwanza duniani kuweza kuchunguza viwango vyote vya mawimbi ya mionzi kwa ajili ya kusimamia hewa na ardhi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako