• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa wito kwa nchi wanachama wa SCO kushirikiana na kuongeza kipato cha sekta ya utalii katika kanda hiyo

    (GMT+08:00) 2018-05-09 17:41:17

    Naibu waziri wa utamaduni na utalii wa China Li Jinzao ametoa wito kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) kutumia fursa na kuzidisha ushirikiano ili kuongeza kipato cha sekta ya utalii katika kanda hiyo.

    Bw. Li amesema hayo kwenye mkutano wa mawaziri wa utalii wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo uliofanyika leo mjini Wuhan, mkoani Hubei. Ametoa mwito kwa nchi wanachama kupanga vizuri maendeleo yao ya sekta ya utalii, kuunganisha mikakati na sera zao za kuendeleza utalii, kuboresha mazingira ya sera za utalii na pia kuhimiza maendeleo ya pamoja ya utalii na sekta husika ili kufanya sekta hiyo itoa manufaa kwa sekta nyingine.

    Naye naibu katibu mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai Aziz Nosirov amesema, kuendeleza sekta ya utalii ni njia muhimu ya kuongeza urafiki na maelewano. Nchi zote wanachama wa Jumuiya hiyo zina rasilimali nyingi za utalii, na zinapaswa kuongeza juhudi ili kuendeleza sekta ya utalii na kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako