• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kongamano la nane la Kimataifa la ununuzi wa umma kufungua uwekezaji

    (GMT+08:00) 2018-05-09 19:50:39
    Kongamano la nane la Kimataifa la ununuzi wa umma linatarajiwa kufungua fursa zaidi za uwekezaji nchini Tanzania.

    Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika jijini Arusha kuanzia Agosti 8 hadi 10 mwaka huu.

    Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,Kamishna wa Sera na Ununuzi wa Umma ,Wizara ya Fedha na Mipango,Dk Fredrick Mwakibinga,alisema lengo la kufanya kongamano hilo ni kuonyesha fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania.

    Alisema kongamano hilo litatumika kutangaza vivutio mbalimbali vya uwekezaji katika sekta ya viwanda na sehemu nyengine.

    Aidha Dk Mwakibinga alisema kongamano hilo pia linalenga kuitangaza Tanzania katika medani za kimataifa,na pia litawakutanisha wataalamu tofauti,na watunga sera kutoka nchi mbalimbali duniani.

    Fauka ya hayo,Dk Mwakibinga alisema wanatarajia kuzalisha ajira kupitia shughuli mbalimbali zitakazokuwa zinaendeshwa katika kipindi chote cha kongamano hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako