• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda itakuwa mwenyeji wa mkutano wa African Green Revolution Forum 2018

    (GMT+08:00) 2018-05-09 19:51:13
    Rwanda itakuwa mwenyeji wa mkutano wa African Green Revolution Forum 2018 (AGRF), jukwaa muhimu ambalo husukuma ajenda ya maeguzi ya kilimo barani Afrika.

    Tangazo hili lilitolewa jana katika kongamano la Transform Africa Summit jijini Kigali.

    Jukwaa la kila mwaka la Kilimo huandaliwa na shirika la Alliance for Green Revolution in Africa (AGRA) na linatarajiwa kufanyika tarehe 3-7 Septemba.

    Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Rwanda kuwa mwenyeji wa mkutano huo.

    Rais wa shirika la AGRA,Agnes Kalibata, aliwaambia waandishi wa habari kwamba kaulimbiu ya mkutano wa mwaka huu ni "Ongoza,pima,kua:Kuwezesha njia mpya za kubadilisha wakulima wadogo kufanya kilimo biashara endelevu".

    Kalibata ,ambaye ni Waziri wa Kilimo wa zamani Rwanda,alisema nchi hiyo ilichaguliwa kuandaa mkutano huo kutokana na juhudi zake za uongozi katika kubadilisha kilimo nchini humo na barani kote.

    Wakati wa mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa,Ethiopia,mwezi Januari mwaka huu,Rwanda ilitambuliwa kama nchi inayofanya vizuri barani Afrika katika malengo ya kilimo kwa kuandikisha jumla ya alama 6.1 chini ya 10.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako