• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wabunge waishauri serikali kupunguza bei ya sukari,iwe kama Zanzibar

    (GMT+08:00) 2018-05-09 19:51:34
    Spika wa bunge la Tanzania,Job Ndugai,ameiagiza serikali kutoa majibu ya uhakika kuhusu utofauti ya bei ya sukari uliopo kati ya Tanzania bara na Zanzibar.

    Agizo la Spika limetokana na baadhi ya wabunge jana kuhoji tofauti hiyo na kuishauri serikali kupunguza bei ya bidhaa hiyo hasa katika kipindi hiki cha kuelekea mwezi Mtukufu wa Ramadhan iwe kama Zanzibar.

    Ndugai alisema suala la sukari ni la msingi sana kwa maisha ya wananchi wa Tanzania na halijapata majibu ,hivyo litapangwa tena wiki ijayo na serikali iandae majibu ya uhakika kwa kuwa watanzania hawawezi kununua sukari kwa bei mara mbili ya Zanzibar kwa sababu tu ya kulinda viwanda.

    Msisitizo huo wa Spika ulitokana na swali la nyongeza la mbunge wa Mpendae,Salim Hassan Turky ,kuhoji serikali kama haioni haja ya kuiga Zanzibar kupunguza bei ya sukari kwa kuwa kuna kiwanda kimoja na sukari mfuko unauzwa Sh65,000 tofauti na Sh110,000 inayouzwa bara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako