• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ligi Kuu Uingereza (EPL): Chelsea yaiombea mabaya Liverpool

    (GMT+08:00) 2018-05-10 09:24:29
    Usiku wa Mei 9 ligi kuu ya Uingereza imeendelea kwa michezo 4 kuchezwa, huku timu nyingi zimebakiwa na mechi moja moja kabla ligi hiyo kumalizika, lakini vita ipo ni timu gani zitapata nafasi ya kucheza Champions League.

    Klabu ya Tottenham Hotspurs baada ya kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Newcastle United sasa ni rasmi wamekata tiketi ya kucheza michuano ya UEFA Champions League msimu ujao na vita ya nafasi moja iliyosalia wameiachia Chelsea na Liverpool.

    Matokeo ya michezo ya ligi hiyo iliyopigwa jana ni Chelsea imetoka sare ya goli 1-1 dhidi ya Huddersfield Town, Leicester City ikiichabanga Arsenal 3-1, Manchester City imeipiga Brighton & Hive Albion 3-1 na mechi ya mwisho ni kati ya Tottenham ilipokumbana na Newcastle.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako