• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Nguvu za uokoaji za kiraia zakua nchini China katika miaka 10 iliyopita baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi la Wenchuan

  (GMT+08:00) 2018-05-10 18:18:57

  Mei, 12 ni siku ya kumbukumbu ya miaka 10 tangu kutokea kwa tetemeko la ardhi la Wenchuan, pia ni "Siku ya Kitaifa ya Kuzuia na Kudhibiti Maafa" iliyoanza kuadhimishwa China miaka kumi iliyopita. Ili kuinua uwezo wa kuzuia na kudhibiti maafa na kuinua mwamko wa jamii nzima na uwezo wa umma wa kujiokoa na kusaidiana, wilaya ya Aba ya mkoa wa Sichuan tarehe 9, Mei ilifanya mazoezi ya kukabiliana na hali ya dharura kutokana na maafa ya kimaumbile ya mtiririko wa mto Min mwaka 2018" katika wilaya ya Wenchuan, Mao na Songpan.

  Mazoezi hayo yaliweka mfano wa kutokea kwa tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 7.0 katika kipimo cha Richtar saa 2 asubuhi ya tarehe 9, Mei mwaka 2018, na kiini cha tetemeko hilo katika kitongoji cha Yingxiu wilayani Wenchuan. Shughuli zilizofanywa ni pamoja na kujiepusha na maafa na kuhamishia watu kwenye maeneo salama, kuita nguvu za uokoaji ndani ya mufa mfupi, kupitisha barabara zinazozuiliwa, uokoaji wa angani, majini, matibabu, kushughulikia vitu vyenye hatari na kuwapanga watu katika nyumba za muda. Kiongozi wa timu ya uokoaji ya Hongyi ya mji wa Nancho iliyoshiriki kwenye mazoezi hayo He Xi ana uzoefu wa miaka 11 wa uokoaji, na alishiriki kazi za uokoaji katika tetemeko la ardhi la Wenchuan la mwaka 2008 na maafa mengine mengi, pia ameshuhudia ukuaji wa nguvu za uokoaji za umma katika miaka hii 10 nchini China. Anasema,

  "Timu ya uokozi inayoundwa na watu wengi wanaojitolea inakabiliana na maafa kwa haraka zaidi kuliko timu ya uokozi ya taifa. Inaweza kufika katika sehemu iliyotokea maafa na kuanza uokoaji wa awali, halafu kusaidia timu ya uokozi ya taifa kufanya uokoaji zaidi."

  He Xin amesema miaka 10 iliyopita, wengi wa wanaojitolea katika kazi za uokoaji kufuatia tetemeko la ardhi la Wenchuan walikuwa na lengo la kuwasaidia wengine, lakini hivi sasa, nguvu za uokoaji za umma zimeboreka na kuongeza uwezo wao katika kazi za uokozi.

  Kushughulikia matatizo ya kisaikolojia baada ya maafa ni kazi muhimu katika shughuli za kuzuia na kudhibiti maafa. Aliyeshiriki kwenye kazi hiyo baada ya tetemeko la ardhi la Wenchuan mshauri wa saikolojia Li Ningjia anasema miaka 10 iliyopita, China haikuwa na mfumo kamili wa kushughulikia msukosuko wa kisaikolojia baada ya maafa na washauri wa kisaikolojia hawakujua jinsi ya kushughulikia matatizo ya kisaikolojia baada ya maafa. Baada ya kujifunza na kufanya majumuisho, sasa kumekuwa na mfumo unaopevuka ambao umepata ufanisi mzuri.

  "kumekuwa na maendeleo makubwa katika kushughulikia matatizo ya kisaikolojia baada ya maafa katika miaka 10 iliyopita. Mwanzoni, hatukuwa na uzoefu, lakini tulihifadhi nyaraka nyingi baada ya tetemeko la ardhi la Wenchuan na tumekuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu saikolojia ya waathirika wa maafa. Sasa baada ya kuingia katika maeneo yaliyotokea maafa, kwanza tunawasiliana na timu ya uokozi. Pia tunazungumza na waathirika wa maafa, na baada ya kupata habari za kimsingi, tunapanga mipango usiku. Kisha tutajua ni nani wanahitaji msaada wa kisaikolojia na ni msaada wa kiwango gani."

  Katika miaka 10 iliyopita, mashirika ya uokoaji ya kiraia ya China yamekua kwa kasi na ufundi umeboreshwa, na yameshiriki kwenye shughuli mbalimbali za uokoaji za kimataifa. Timu za uokozi za kiraia za China zimeonekana katika shughuli za uokoaji kufuatia tetemeko la ardhi la Nepal, maafa ya upepo ya Ufilipino na tetemko la ardhi la Ecuador. Katibu mkuu wa Mfuko wa Ustawi wa Umma wa Pinglan wa Beijing Wang Yingjie anasema,

  "Tokea mwaka 2012, tumeanza kushirikisha timu za uokozi za kiraia za China, na kuzipeleka katika nchi zilizo katika 'Ukanda Mmoja, Njia Moja" ili kuzisaidia kukabiliana na maafa, kuanzisha mfumo wenye ufanisi wa kupunguza na kuzuia maafa na kuyasaidia mashirika yao ya kiraia kukua."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako