• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matumizi ya mtandao wa 4G yafikia asilimia 94

  (GMT+08:00) 2018-05-10 19:43:23
  Katika mda wa miaka 4 tu tangu kuanzishwa kwa matumizi ya mtandao wa 4G ,Rwanda imefikisha huduma hiyo kwa watu asilimia 94.

  Mkurugenzi mkuu wa kongamano la mageuzi ya Afrika Rwanda Patrick Yoon amesema licha ya changamoto za hapa na pale katika kuafikia malengo yao,juhudi na ushirikiano na serikali ya Korea wamefikia walengwa na kuboresha biashara kupitia kwa teknolojia ya mtandao huo wa kasi.

  Rwanda imekuwa nchi ya kwanza barani Afrika kufikisha mtandao wa 4G katika mikoa yote .

  Washikadau wa sekta ya mitandao na biashara nchini Rwanda wanasema nchi hiyo itaingia miongoni mwa nchi zitakazopata mabadiliko makuu ya viwanda kwa kuimarisha matumizi ya teknolojia.

  Mtandao huo umechangia kubuni ajira na huduma mpya katika sekta ya mawasiliano.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako