• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kuvuta sigara kunaweza kuzuiwa zaidi katika kujikinga na magonjwa ya moyo na mishipa ya damu

    (GMT+08:00) 2018-05-11 17:43:25

    Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa cha China kimetoa taarifa kuwa kuvuta sigara au moshi kutoka kwa mvutaji mwengine vinaweza kuzuiwa zaidi katika kujikinga na magonjwa ya moyo na mishipa ya damu.

    Naibu mkurugenzi wa Kituo hicho Li Xinhua amesema magonjwa hayo yamesababisha vifo na ulemavu kwa watu wengi zaidi kuliko magonjwa mengine duniani, ambapo nchini China vifo vinavyotokana na magonjwa ya moyo na mishipa ya damu vimechukua asilimia zaidi ya 40 ya vifo vyote. Anasema,

    "Kuvuta sigara kunaweza kudhuru moyo na kuongeza hatari ya kupata ugonjwa wa moyo. Takwimu zimeonesha kuwa kuvuta sigara moja kila siku kunaweza kuongeza hatari ya kupata ugonjwa huo kwa asilimia 74 kwa wanaume huku ikiwa asilimia 119 kwa wanawake. Hizi ni takwimu muhimu sana."

    Mwaka 2003, China ilisaini Mkataba wa Utaratibu wa Kudhibiti Tumbaku wa Shirika la Afya Duniani WHO, na ulianza kutekelezwa rasmi mwaka 2006. Hadi sasa miji zaidi ya kumi nchini China ikiwemo Beijing, Shanghai na Shenzhen imetekeleza sheria ya kutovuta sigara kwenye sehemu za wazi, ambao imewafikia asilimia kumi ya watu wote wa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako