• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bei ya mchela yapanda Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-05-11 19:20:35

    Bunge la Tanzania limeelezwa kuwa, katika mwaka 2017/2018 bei ya mazao makuu ya chakula hasa mahindi, maharage na mchele zimeshuka na kupanda kwa viwango tofauti ikilinganishwa na msimu wa 2016/2017.

    Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma.

    Amesema bei ya gunia la mchele la kilo 100 iliongezeka kutoka wastani wa shilingi 174,316 msimu wa 2016/2017 hadi shilingi 195,201 msimu wa 2017/2018 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 11.98.

    Waziri Mwijage amesema ongezeko hilo la bei ya mchele linatokana na ongezeko la mahitaji kwa zao hilo ikilinganishwa na uzalishaji wake. Amesema, kwa wastani be ya gunia la mahindi la kilo 100 ilipungua kutoka shilingi 98,077 hadi 49,386 ikiwa ni sawa na upungufu wa 49.65%.

    Bei ya jumla ya maharage kwa gunia la kilo 100 ilishuka kutoka shilingi 178,070 mwaka 2016/2017 hadi kufikia shilingi 169,771 mwaka 2017/2018, sawa na upungufu wa asilimia 4.66.

    Amesisitiza kuwa kushuka kwa bei za mahindi na maharage kumesababishwa na ongezeko la uzalishaji kwa kutokana na hali ya hewa nzuri mwaka 2017/2018.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako