• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali ya Tanzania yatangaza malengo ya sekta ya viwanda mwaka wa fedha wa 2018/2019

  (GMT+08:00) 2018-05-11 19:21:29

  Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji imetangaza malengo ya sekta ya viwanda katika mwaka wa fedha 2018/2019.

  Waziri wa Wizara hiyo Bw. Charles Mwijage ameyataja malengo hayo kuwa ni pamoja na kufanya tathmini ya sekta ya sukari, kutathmini ya sekta ya mafuta ya kula na kufanya tathmini ya sekta ya vifaa vya ujenzi.

  Aidha Mwijage ametaja malengo mengine kuwa ni kutathmini ya sekta ya chuma, kufanya tathmini ya sekta ya mbao na bidhaa za mbao, na kuitathmini sekta ya ngozi na bidhaa za ngozi.

  Malengo mengine ni kufanya tathmini ya sekta ya nguo na mavazi huku yote hayo yakifanywa kwa kutathmini hali halisi ya uzalishaji viwandani na mahitaji ya bidhaa.

  Mengine ni kuitathmini sekta ya usindikaji vyakula ukiwemo mchele, unga, mbaazi na vyakula vingine.

  Malengo mengine ni kutathmini usindikaji vyakula vya binadamu na wanyama na pia kufanya tathmini ya dawa za binadamu, vifaa tiba, na vifungashio. Mwijage amesema, kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, hadi Machi mwaka huu, Tanzania ilikuwa na viwanda 53,876 vikiwemo vikubwa 251.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako