• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vikundi 16 vya vijana vyaunda kwa ajili ya kusaidika kibiashara Kenya

    (GMT+08:00) 2018-05-11 19:21:50

    Viongozi wa Kaunti ya kiambu nchini Kenya wamesema haja ya kutatua shida ya ukosefu wa ajira ili kukabiliana na umaskini katika eneo hilo.Viongozi hao wameahidi kushirikiana na serikali na sekta ya kibinafsi ili kuangazia maswala ya ajira katika eneo hilo. Wamesema hiyo ndiyo njia ya kipekee ya kuwasaidia wananchi kujiendeleza kwa kujitafutia ajira ambapo maisha ya kila mmoja yatainuka..

    Tayari viongozi hao kwa kushirikiana na serikali ya kaunti ya Kiambu wamebuni vikundi tofauti kwa ajili ya kuvifadhili kibiashara. Aidha viongozi hao wameeleza kuwa sababu iliyopelekea kuchukua hatua hiyo ni kuwa kuajiriwa ofisini sio suluhisho la kukidhi matakwa ya kila mmoja kwa hiyo ni vyema kubuni njia nyingine ya kuwafaidisha wananchi.

    Zaidi ya vikundi 16 vya kujiendeleza kibiashara vimebuniwa katika kaunti hiyo na hivi sasa vinafanya vizuri katika biashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako