• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi Jinping atuma barua kwa semina ya kimataifa ya kukumbusha tetemeko la ardhi la Wenchuan

  (GMT+08:00) 2018-05-12 14:43:38

  Semina ya kimataifa ya kukumbusha miaka 10 tangu kutokea kwa tetemkeo la ardhi la Wenchuan ambayo pia ni semina ya kimataifa kuhusu matetemeko ya ardhi ya China Bara leo imefunguliwa mjini Chengdu, China, na rais Xi Jinping ametuma barua kwa semina hiyo.

  Rais Xi amesema huu ni mwaka wa 10 tangu kutokea kwa tetemeko kubwa la ardhi la Wenchuan, chini ya uongozi imara wa Chama cha Kikomunisti cha China, ukarabati wa sehemu zilizoathiriwa na tetemeko hilo umepata mafanikio makubwa, na kutoa uzoefu mzuri kwa kazi za ukarabati baada ya matetemeko ya ardhi duniani.

  Rais Xi pia amesema, China itafuata mawazo ya maendeleo yanayozingatia zaidi maslahi ya wananchi, na kujiongezea uwezo wa kukabiliana na maafa, ili kuhakikisha usalama wa mali na maisha ya wananchi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako