• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China atoa rambirambi kwa rais wa Kenya kutokana na vifo vilivyosababishwa na kubomoka kwa kuta za bwawa

  (GMT+08:00) 2018-05-12 20:27:28

  Rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za rambirambi kwa rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kutokana na janga la kubomoka kwa kuta za bwawa ambayo limesababisha vifo na majeruhi ya watu wengi.

  Kwenye salamu zake, rais Xi amesema kwa niaba ya serikali, watu wa China na yeye binafsi, anatoa rambirambi kwa watu waliofariki na kuwapa pole wafiwa na majeruhi. Amesema anaamini kuwa chini ya uongozi wa rais Uhuru na serikali ya Kenya, watu walioathiriwa watashinda matatizo yote, na kurejesha maisha ya kawaida mapema.

  Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi siku hiyo pia ametoa salamu za rambirambi kwa mwenzake wa Kenya Monica Juma kuhusu janga hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako