• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mataifa ya Afrika U-20: Burundi yapata sare, Rwanda na Tanzania zashindwa nyumbani

  (GMT+08:00) 2018-05-14 10:36:15

  Ikiwa nyumbani mjini Bujumbura, Timu ya taifa ya Burundi mwishoni mwa juma imelazimishwa matokeo ya sare ya magoli 1-1 na Sudan kwenye mechi za raundi ya pili za kufuzu mashindano ya Afrika ya Mwaka 2019 yatakayofanyika nchini Niger.

  Goli la Burundi lilifungwa na Djuma Muhamedi katika dakika ya 20 kabla ya Eldin Musa kusawazisha kunako dakika ya 29.

  Habari ilikuwa mbaya kwa timu nyingine za Afrika mashariki, ambapo Rwanda ikiwa kwenye uwanja wa nyumbani mjini Kigali ilifungwa na Zambia kwa magoli 2-1, na Tanzania ilikubali kufungwa 2-1 na Mali ikiwa nyumbani mjini Dar es Salaam.

  Matokeo hayo sasa yanaziweka katika mazingira magumu timu hizo, kwa kuwa zitalazimika kupata ushindi ugenini ili kufuzu, na mechi za marudiano zitachezwa mwishoni mwa juma hii.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako