• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wachezaji wa Afrika Mashariki wang'ara Ulaya: Wanyama (Kenya) na Samatta (Tanzania)

    (GMT+08:00) 2018-05-14 10:36:45

    Katika mechi zilizopigwa jana barani Ulaya wachezaji wa kulipwa kutoka Afrika Mashariki Mbwana Samatta kutoka Tanzania na Victor Wanyama wa kutoka Kenya wameng'ara vilivyo baada ya kila mmoja kuisaidia timu zao kupata ushindi muhimu.

    Samatta ambaye amerejea baada ya kuwa majeruhi, jana amefunga magoli mawili wakati timu yake ya KRC Genk ilipopata ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya Charleroi kwenye mechi za hatua ya mwisho wa ligi kwa ajili ya kupata timu zitakazoshiriki ligi ya klabu bingwa ulaya na ligi ya Yuropa.

    Kwa upande wake Victor Wanyama, takwimu za mchezo wa jana ambao timu yake ya Tottenham Hotspurs ilipata ushindi dhidi ya Leceister City na kuiweka katika mazingira salama ya kucheza ligi ya klabu bingwa ulaya msimu ujao, zinaonyesha kuwa alikuwa mchango kutokana na kudhibiti vyema nafasi ya kiungo, lakini vilevile akitoa usaidizi (assists) uliopelekea magoli kupatikana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako