• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yaendelea kutamba kwenye Kombe la Dunia kwa Vijana wanaoishi kwenye mazingira hatarishi

    (GMT+08:00) 2018-05-14 10:37:17

    Timu ya Wasichana ya Tanzania inayoshiriki mashindano ya kombe la dunia kwa watoto wanaoishi mazingira hatarishi (Street Child World Cup), yalioandaliwa na shirika la Street Child United kwa programu yake iitwayo 'Future Depends on You' mwishoni mwa juma hili imefuzu hatua ya nusu fainali.

    Timu hiyo ilifuzu kwa nusu fainali baada ya kuishinda Marekani kwa magoli 5-0 kwenye mechi ya wa Robo fainali na ikakutana na Uingereza kwenye nusu fainali.

    Tanzania ilifuzu nusu fainali ikiwa haijapoteza hata mchezo mmoja na ikiwa haijafungwa hata goli moja yani clean sheet katika mashindano hayo yanayofanyika mjini Moscow.

    Timu hiyo ndiyo mabingwa watetezi wa mashindano hayo, kwani mwaka 2014 ndiyo iliyoshinda ubingwa nchini Brazil .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako