• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashindano ya Magari ya Mwendokasi, Hamilton ashinda nafasi ya kwanza kwa mara ya pili mfululizo

    (GMT+08:00) 2018-05-14 10:38:01

    Dereva Lewis Hamilton ameendeleza rekodi ya kushinda baada ya kushika nafasi ya kwanza kwenye mashindano ya magari ya mwendokasi ya Barcelona jana nchini Hispania.

    Katika mbio hizo, nafasi ya pili ilikwenda kwa dereva mwenzake wa Mercedes, Valterri Bottas wa Finland, na nafasi ya tatu ikichukuliwa na Max Verstappen wa Ubelgiji na timu ya Redbull.

    Mpinzani wa Karibu wa Lewis, ambaye ni dereva wa Ferari, mjerumani Sebastian Vettel jana alishika nafasi ya 4.

    Ushindi huu pamoja na ule aliopata Aprili 29 nchini Azerbaijan, unamuongezea alama muhimu kwa ajili ya kushinda ubingwa wa jumla kwenye mashindano hayo msimu huu.

    Madereva hao sasa wanajiandaa na mashindano ya Monaco-Ufaransa, Mei 27.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako