• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ligi Kuu ya Uingereza: msimu wa mwaka 2017-2018 wamalizika rasmi jana 

  (GMT+08:00) 2018-05-14 10:38:47
  Jana kumepigwa mechi kumi za mwisho za ligi kuu ya nchini Uingereza ambazo zilitoa hatma ya timu hizo kwenye msimamo wa ligi, ambapo Man City, Man United, Tottenham na Liverpool zilipata ushindi lakini ukiwa muhimu zaidi kwa Liverpool kwani uliifanya ikae katika nafasi muhimu nne bora za juu.

  Hata hivyo, kutokana na Chelsea kufungwa kwenye mechi yake ya jana na Newcastle United kungeifanya Liverpool ipate fursa hiyo hata kama ingefungwa.

  Lakini Manchester City jana imejewekea rekodi nyingine jana, ikiwemo kupata pointi 100, ikiwa ni 19 zaidi ya timu inayoshika nafasi ya pili.

  Pia imevunja rekodi ya ushindi mara 32, lakini ikimaliza ligi kwa kuwa na tofauti kubwa kati ya magoli ya kufunga na kufungwa ambayo ni 79.

  Kwa upande mwingine, Mchezaji wa kimataifa wa Misri Mohamed Salah amevunja rekodi ya ufungaji wa magoli mengi katika ligi kuu ya Uingereza baada ya kufikisha 32 ikiwa ni moja zaidi ya aliyofunga Luis Suarez msimu wa 2013-2014, Cristiano Ronaldo 2007-2008 na Alan Shearer 1995-1996.

  Zaidi Salah, alitangazwa mfungaji bora na mchezaji bora kwa msimu huu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako