• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mjumbe maalumu wa rais wa Xi Jinping wa China afanya ziara nchini Marekani kufanya mazungumzo

  (GMT+08:00) 2018-05-14 15:47:07
  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang leo ametangaza kuwa, kutokana na mwaliko wa serikali ya Marekani, mjumbe maalumu wa rais Xi Jinping wa China, mjumbe wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China, naibu waziri mkuu wa China ambaye pia ni kiongozi wa China wa mazungumzo ya kiuchumi kati ya China na Marekani Bw. Liu He atafanya ziara nchini marekani kuanzia tarehe 15 hadi tarehe 19 Mei.

  Wakati wa ziara yake, Bw. Liu He ataendelea na mazungumzo na kundi la Marekani linaloongozwa na waziri wake wa fedha Bw. Steven Mnuchin kuhusu suala la uchumi na biashara kati ya nchi hizo mbili.

  Bw. Lu Kang amesema kuwa, China inapenda kushirikiana na Marekani kufanya juhudi kuhimiza mazungumzo hayo kupata matokeo mazuri na ya kiujenzi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako