• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika kutoa mchango muhimu kwa uhusiano kati ya pande hizo mbili

  (GMT+08:00) 2018-05-14 16:34:25

  Balozi mpya wa China nchini Kenya Bibi Sun Baohong amewasili Nairobi na kuanza kazi zake nchini Kenya. Baada ya kuwasili Bibi Sun alisema hivi sasa uhusiano kati ya China na Kenya ni mzuri zaidi katika historia, akiwa balozi wa China nchini Kenya, atashirikiana vizuri na Kenya kuhimiza uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati katika pande zote kati ya nchi hizo mbili.

  Bibi Sun alipozungumzia matumaini yake kuhusu maendeleo ya uhusiano kati ya China na Kenya, na namna ya kuhimiza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, anasema,

  "Katika miaka kadhaa iliyopita, uhusiano kati ya China na Kenya umepata maendeleo makubwa. Mwaka jana kwenye mkutano wa kilele wa ushirikiano wa kimataifa wa "Ukanda Moja, Njia Moja", rais Xi Jinping wa China na rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kwa kauli moja walikubali kuinua kiwango cha uhusiano kati ya nchi hizo mbili kuwa uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote. Nikiwa balozi wa China nchini Kenya, nitashirikiana vizuri na Kenya, ili kuhimiza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika nyanja mbalimbali."

  Bibi Sun anaona baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika ni mfumo muhimu wa pande hizo mbili kufanya mazungumzo na ushirikiano, na pia ni bendera ya kuhimiza ushirikiano kati ya Afrika na nchi nyingine za dunia. Mkutano wa kilele wa baraza hilo utakaofanyika mwezi Septemba mjini Beijing utatoa mchango muhimu kwa maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika na China na Kenya. Anasema,

  "Mkutano huo ni muhimu sana. Viongozi wa China na nchi za Afrika watakutana mjini Beijing kujadili mipango ya ushirikiano wa kirafiki, kuanzisha jumuiya yenye mustakabali wa pamoja, na hatua za kutekeleza pendekezo la "Ukanda Mmoja,Njia Moja".

  Alipozungumzia mawasiliano kati ya wananchi wa China na Kenya, Bibi Sun anasema,

  "Mawasiliano ya ustaarabu ni moja ya nguzo tano za uhusiano kati ya China na Afrika, huku mawasiliano ya watu ukiwa mwanzo wa kukuza ushirikiano. Mawasiliano ya ustaarabu na watu kati ya China na Kenya yana msingi mzuri, na yanaweza kuendelezwa zaidi. Katika miaka ijayo, tutajumuisha rasilimali za makampuni, mashirika ya habari, taasisi ya Confucius ya China nchini Kenya pamoja na watalii wa China, kuanzisha majukwaa ya ushirikiano, ili kuhimiza mawasiliano hayo kupata maendeleo zaidi, na kuwanufaisha watu wa nchi hizo mbili."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako