• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Utafiti wasema uchomaji wa makaa ya mawe sio chanzo kikuu cha uchafuzi mjini Beijing

  (GMT+08:00) 2018-05-14 18:48:11

  Utafiti uliofanywa na Mamlaka ya Ulinzi wa Mazingira ya Beijing umeonyesha kuwa, uchomaji wa makaa ya mawe sio tena chanzo kikuu cha PM2.5 mjini Beijing, bali hewa chafu inayotolewa na magari imechukua nafasi ya juu.

  Matokeo hayo yamekuja wakati Beijing inasisitiza matumizi ya gesi asilia badala ya makaa ya mawe kwa ajili ya kuleta joto wakati wa msimu wa baridi na kufunga viwanda vinavyoleta uchafuzi wa hewa.

  Uchafu unaotoka kwenye magari, meli na mashine za ujenzi ni vyanzo vikuu vya PM2.5, vikichangia asilimia 45 ya jumla ya vyanzo vya uchafuzi wa hewa mjini Beijing.

  Kiwango cha PM2.5 mjini Beijing kimepungua na kufikia kiwango cha chini zaidi kuanzia mwaka 2013 wakati kampeni ya kitaifa ya kudhibiti uchafuzi wa hewa ilipoanza.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako