• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya Watumishi wa umma kuanzia mwezi Oktoba mishahara yao itapunguzwa na asilimia 7.5 ajili ya mchango wao wa pensheni

    (GMT+08:00) 2018-05-14 19:14:57
    Watumishi wa umma kuanzia mwezi Oktoba mishahara yao itapunguzwa na asilimia 7.5 kwa ajili ya mchango wao wa pensheni.

    Waziri wa fedha Henry Rotich ametangazia Bunge, kwamba kucheleweshwa kwa mpango wa mfumo wa pensheni utaanza mwezi Oktoba Kenya iking'ang'ana kufikia gharama za kustaafu za watumishi wa umma.

    Serikali itatekeleza mpango wa pensheni kuanzia mwezi Oktoba 2018.

    Serikali imetenga Sh bilioni 15.3 kwa mpango huo, katika mwaka wa fedha 2018/2019, ambao unapaswa kuongezeka hadi Sh bilioni 33.8 bilioni kwa muda mfupi.

    Mpango wa kuchangia pesa, utaona serikali ikiiga mfano wa pensheni ya sekta binafsi pale michango kutoka kwa waajiri na wafanyakazi imewekezwa katika hisa, mali na karatasi ya serikali ili kuzalisha mapato.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako