• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania Serikali yaagiza nje tani 70,000 za sukari

  (GMT+08:00) 2018-05-14 19:16:14

  SERIKALI imeagiza tani 70,354.35 za sukari kutoka nje ya nchi ili kukabiliana na upungufu wa bidhaa hiyo, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

  Waziri wa Kilimo, Dk Charles Tizeba amesema mwishoni mwa wiki kuwa tani 60,539.35 ya sukari itaanza kuingia nchini katikati ya mwezi Mei mwaka huu, ambapo kiasi kilichobaki cha tani 9,815 kitaingia mwezi Juni mwaka huu.

  Aidha, Dk Tizeba amesema hakutarajiwi kuwepo upungufu wa sukari nchini kwa sababu hadi kufikia Mei 10, mwaka huu, katika maghala ya wazalishaji na wafanyabiashara kulikuwa na tani 78,147.67 za sukari na kiasi kingine tani 25,441.25 kipo bandarini kikisubiri kuingia kwa watumiaji.

  Awali, Dk Tizeba alisema mahitaji ya sukari nchi nzima ni tani 630,000 ambapo kati ya hizo tani 145,000 ni kwa ajili ya matumizi ya viwandani na tani 485,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida.

  Hata hivyo, mapitio yanaonesha kwamba msimu wa mwaka 2017/18 viwanda vya ndani vilizalisha tani 306,226 za sukari kwa matumizi ya kawaida ambapo mwisho wa msimu huu, uzalishaji umefikia tani 307,481.76.

  Aidha, Waziri Tizeba alibainisha kuwa kwa kiasi ambacho sukari imeagizwa kutoka nje ya nchi pamoja na viwanda vya ndani, inadhihirisha kwamba hakutakuwa na upungufu wa aina yoyote ya sukari nchini na ikizingatiwa kuwa viwanda vitaanza uzalishaji mwingine mwezi Mei ambapo ukarabati utakuwa umekamilika .

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako