• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Mataifa wapongeza mpango wa Korea Kaskazini wa kufunga eneo la kufanya majaribio ya nyuklia

  (GMT+08:00) 2018-05-15 09:52:21

  Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amepongeza mpango wa Korea Kaskazini kufunga eneo la kufanyia majaribio ya nyuklia nchini humo, akisema hii ni hatua muhimu ya kujenga imani.

  Katika taarifa aliyoitoa katika ziara yake mjini Vienna kwa ajili ya mkutano wa Umoja wa Mataifa, Bw. Guterres amesema mpango huo utachangia juhudi za amani ya kudumu na kitendo halisi cha kufanya Peninsula ya Korea iwe sehemu isiyo na silaha za nyuklia.

  Wikiendi iliyopita, Korea Kaskazini ilitangaza uamuzi wa kufunga maeneo ya kufanya majaribio ya nyuklia yaliyo chini ya ardhi huko Punggye-ri.

  Bw. Guterres pia ameeleza matumaini yake kuwa hatua hiyo chanya kuhusu suala la nyuklia la Peninsula ya Korea, itasaidia mkutano kati ya viongozi wa Marekani na Korea Kusini unaotarajiwa kufanyika mwezi Juni nchini Singapore.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako