• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • EAC: EAC yashindwa kukubaliana kuhusu utoaji wa mchango wa bajeti

  (GMT+08:00) 2018-05-15 18:15:14
  Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zitaendelea kutoa michango sawa ya bajeti, ambapo kila nchi huchangia kwa usawa wa bajeti ya Sekretarieti, baada ya wanachama kushindwa kukubaliana juu ya mfumo bora wa fedha.

  Katika mkutano wake mjini Arusha, Baraza la Mawaziri la EAC likubaliana kushauriana zaidi juu ya njia nzuri ya utoaji wa fedha.

  Tanzania, Kenya na Uganda zinataka kuendelea na mfumo wa sasa, zikisema kuwa nchi zote ni washirika sawa na hivyo zinapaswa kuchangia kwa sawa.

  Lakini Rwanda na Burundi wanapendelea utaratibu tofauti wa utoaji wa mchango, ikiwa ni pamoja na chaguo la utoaji wa kodi za bidhaa kutoka nje.

  Karibu asilimia 57 ya bajeti sawa na dola milioni 56.8 hufadhiliwa na mataifa wanachama, na kila nchi huchangia dola milioni 9 huku asilimia 43 ikichangiwa na washirika wa kimaendeleo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako