• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Benki ya Afrika kutoa mafunzo kwa wafanya biashara

  (GMT+08:00) 2018-05-15 18:16:43
  Benki ya Afrika (Bank of Africa) inalenga kuanza kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara wadogo na wa wastani kwa kuandaa warsha kwao kila mwezi.

  Benki hiyo yenye matawi 30 nchini Kenya imesema mafunzo hayo yatasaidia wafanyabiashara na wateja wake kufahamu fursa mpya hasa kwenye serikali katika sekta kama vile afya, kilimo na utengenezaji bidhaa.

  Mkurungezi wa benki hiyo Ronald Marambii amesema wataalam pia watawasaidia wafanyabiashara kukabili changamoto zinazozuia ukuaji.

  Hatua ya Benki hiyo ni siku chache baada ya ile ya, Ecobank, kuzindua jukwaa ambapo wajasiriamali wanaweza kufanya biashara baina yao kupitia kwa matawi 33 ya benki hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako