• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Mradi wa umeme wa Mto Rufi kuanza Julai

  (GMT+08:00) 2018-05-15 18:17:00
  Waziri wa Nishati, wa Tanzania Dk Medard Kalemani amesema kazi ya ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme kwa nguvu za maji ya Mto Rufi ji eneo la Stiegler's Gorge, unatarajiwa kuanza Julai mwaka huu.

  Dk Kalemani alisema kuwa hatua hiyo ya kuanza kwa mradi inatokana na kazi ya tathmini ya kumpata mkandarasi wa ujenzi kukamilika.

  Akizungumza wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dk Kalemani alisema mradi huo utaanza baada ya taratibu zote za kiutendaji kukamilika, ambako mradi huo mkubwa wa umeme utaongeza megawati 2,100, zaidi ya megawati 560 zinazozalishwa katika miradi mingine ya maji.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako