• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchumi wa China waendelea kwa utulivu katika mwezi wa Aprili

    (GMT+08:00) 2018-05-15 18:26:28

    Ofisi ya habari ya baraza la serikali ya China leo imefanya mkutano na waandishi wa habari kuhusu hali ya maendeleo ya uchumi wa China katika mwezi Aprili. Msemaji wa idara ya takwimu ya China amesema, hali ya uchumi wa China katika mwezi wa Aprili iliendelea kwa utulivu, na China ina uwezo na mazingira ya kudumisha mwelekeo mzuri wa maendeleo ya uchumi.

    Msemaji wa idara ya takwimu ya China Bi Liu Aihua amesema, mwezi uliopita hali ya uchumi wa China ilidumisha mwelekeo mzuri. Anasema,

    "Kwanza shughuli za uzalishaji, haswa wa viwanda ziliongezeka. Katika miezi minne iliyopita, thamani ya uzalishaji viwandani iliongezeka kwa asilimia 9.6 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu, huku thamani ya mauzo ya bidhaa ikiongezeka kwa asilimia 9.7."

    Bi Liu Aihua alipozungumzia hali ya ajira amesema, watu wasio na ajira imekuwa chini ya asilimia 5 katika mwezi uliopita, na kupungua kiasi ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu. Wakati huo huo kiwango cha bei ya bidhaa kimeongezeka kwa kiasi kinachofaa.

    Kuhusu hali ya uchumi katika robo ya pili, Bi Liu Aihua amesema, China ina uwezo na mazingira i ya kudumisha mwelekeo mzuri wa maendeleo ya uchumi. Anasema,

    "Kwanza, kwa hali ya jumla China imeendelea kuboresha muundo wa uchumi na uhusiano wa utoaji na mahitaji. Pili, mapato ya watu wa hali mbalimbali vinaongezeka, na imani ya makampuni na masoko kuhusu hali ya uchumi inaongezeka."

    Bi Liu Aihua amesema China ina soko kubwa zaidi duniani, inakamilisha miundombinu yake haswa reli na barabara za mwendo kasi, na kiwango cha akiba ya pesa ya wananchi katika benki ni cha juu. Hali hizo zinahakikisha uchumi wa China unaendelea vizuri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako