• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Burundi yaitaka DRC kushikiana nayo katika kuwakamata watuhumiwa wa shambulizi la mauaji

  (GMT+08:00) 2018-05-15 19:12:01

  Burundi imeitaka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kushirikiana nayo ili kuwakamata wapiganaji walioua watu 26 kaskazini magharibi mwa Burundi.

  Mwanasheria Mkuu wa Burundi Sylvestre Nyandwi amesema, uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa wahalifu waliofanya mauaji hayo walikimbilia DRC. Amesema tayari imeanzishwa tume ya uchunguzi ambayo imepewa mwezi mmoja kumaliza uchunguzi wake, na pia katika mwezi huo, tume hiyo inatakiwa kufungua mashtaka.

  Wapiganaji hao walishambulia kijiji kimoja kilichoko wilaya ya Buganda, mkoa wa Cibitoke jumamosi iliyopita na kuua watu 24 papo hapo na wengine wawili kufia hospitali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako