• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Baraza la Usalama la UM lakubali kurefusha muda wa tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia

  (GMT+08:00) 2018-05-16 09:47:19

  Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio la kukubali kurefusha muda wa tume ya kulinda amani ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM, ili kutoa muda wa kupitia ripoti ya tathmini kabla ya idhini ya muda mrefu zaidi.

  Azimio nambari 2415 lililopitishwa na nchi 15 wajumbe wa baraza hilo limerefusha muda wa AMISOM hadi Julai 31 mwaka huu.

  Muda wa sasa wa tume hiyo utakwisha Mei 31. Baraza la Usalama lilitarajia matokeo ya tathmini ya pamoja ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kabla ya kufanya uamuzi kuhusu kurefusha muda wa tume hiyo.

  Lakini tathmini hiyo imecheleweshwa na ripoti haitatolewa mpaka Juni 15. Hali hiyo imelilazimisha baraza hilo kupanga kurefusha muda wa tume hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako