• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi asisitiza uongozi mkuu wa CPC katika masuala ya kigeni

    (GMT+08:00) 2018-05-16 09:51:31

    Katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC Xi Jinping ametoa wito wa kuimarisha uongozi mkuu wa Kamati hiyo katika masuala ya kigeni, na kujenga mustakbali mpya wa diplomasia kati ya nchi kubwa yenye umaalumu wa kichina, ili kusaidia kutimiza malengo mawili ya miaka 100 na ndoto ya wachina ya kustawisha tena taifa lao.

    Bw. Xi ametoa kauli hiyo alipokuwa akiendesha mkutano wa kwanza wa Tume ya Masuala ya Kigeni ya Kamati Kuu ya CPC. Amesema China imefanya uvumbuzi kuhusu nadharia na uzoefu wa kidiplomasia, kuboresha diplomasia ya pande nyingi, kuhimiza ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na kujihusisha kwa kina katika mageuzi na ujenzi wa mfumo wa uongozi wa kimataifa tangu mkutano mkuu wa 18 wa CPC ufanyike mwaka 2012.

    Pia amesema katika dunia ya leo isiyo na uhakika na utulivu, mbali na fursa, maendeleo ya China pia yanakabiliwa na changamoto, na amezitaka idara husika za chama zifuatilie vizuri mabadiliko ya hali ya kimataifa, kuwa na upeo wa mbali na kushughulikia ipasavyo changamoto hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako