• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kituo cha CCS kukuza ushirikiano China na Tanzania,asema waziri Dk Augustine Mahiga

  (GMT+08:00) 2018-05-16 19:24:31
  Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki,Dk Augustine Mahiga,amesema ufunguzi wa Kituo cha Taaluma za China (CCS) kilichopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam utaimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi uliopo baina ya nchi hizo mbili.

  Aidha Waziri Mahiga aliwataka watanzania kutumia CCS kujifunza mbinu ilizotumia China kupiga hatua kubwa kimaendeleo kwa muda mfupi.

  Alisema kupitia chuo hicho cha China ,UDSM itanufaika kwa kutoa elimu,kufanya tafiti,na kukuza utekelezaji wa mahusiano ambayo viongozi waasisi wa nchi hizo walianzisha.

  Dk mahiga aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizindua kituo hicho na kueleza kuwa China imepiga hatua kimaendeleo na kiuchumi hivyo ni fursa ya kipekee kwa watanzania kubadilisha mtazamo kwa kujifunza kupitia nchi hiyo.

  Pia alisema ipo misaada ya moja kwa moja ambayo China inaipatia Tanzania katika sekta mbalimbali zikiwamo kilimo,afya,elimu na miundombinu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako