• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya-Ripoti ya Benki ya Dunia yaonyesha kuwa motto wa tajiri ana nafasi nzuri maishani

  (GMT+08:00) 2018-05-16 19:24:51
  Mtoto anayezaliwa katika familia maskini nchini hupata nafasi ndogo ya kujiimarisha kiuchumi kuliko yule anayezaliwa katika familia inayojiweza kimapato, ripoti imebainisha.

  Ripoti hiyo iliyotolewa na Benki ya Dunia inasema kwamba hali hii husababishwa sana na ukosefu wa sera bora ambazo zinaweza kutoa nafasi sawa kwa kila mwananchi kujiinua kimaisha.

  Miongoni mwa mataifa 75 yaliyofanyiwa utafiti, Kenya iliorodheshwa kati ya 25 za mwisho pamoja na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC), Mali, Malawi, Uganda, Nigeria, Africa Kusini, Colombia, Ecuador, Guatemala na Panama.

  Ingawa watafiti walikiri kwamba mataifa 75 ulimwenguni ni machache kwa kutambua hali halisi ilivyo, walisema matokeo ya utafiti huo ni muhimu kwa mataifa mbalimbali yanayokua kiuchumi.

  Ripoti hiyo iliyoandikwa na kikundi cha watafiti na wachanganuzi wakiongozwa na Ambar Narayan na Roy Van der Weide, ilisema wakati mwingi hali hii husababishwa na jinsi hakuna sera za kuleta usawa wa kimapato na elimu katika jamii.

  Ili kubadili hali, ilipendekezwa kuwa mataifa yaunde nafasi sawa kwa minajili ya kuondoa changamoto zinazokumba watu binafsi na familia wanapojaribu kujiimarisha kiuchumi.

  Ilibainika tofauti zilizopo huwa katika masuala kama vile kiwango cha elimu cha anayesimamia familia, eneo ambapo watu wanaishi (mjini au mashambani), utajiri wa familia, hali halisi ya mtoto na hali ya watu walio katika familia.

  Hata hivyo, Kenya ilisifiwa kwa juhudi zake za kupambana na ukosefu wa usawa katika elimu kama njia ya kupitia kwa mipango ya kuangamiza minyoo kwa watoto na kupeana chakula bila malipo shuleni.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako