• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda kupata ukuaji mzuri wa uchumi,yasema Benki ya Dunia

  (GMT+08:00) 2018-05-16 19:25:48
  Benki ya Dunia imesema Uganda inatarajiwa kupata ukuaji zaidi kutokana na mvua ambazo zimeongeza mazao ya kilimo,na ukuaji wa miundombinu ya mafuta wakati nchi hiyo ikijiandaa kwa uzalishaji wa mafuta kwa ajili ya biashara.

  Kulingana na mwanauchumi wa Benki ya Dunia ,Rachel Sebudde,Uchumi unatarajiwa kuongezeka hadi asilimia 5.5% mwkaa huu wa fedha na baadae kukua hadi 6% katika mwaka wa fedha 2018/19.

  Ofisi ya Takwimu ya Uganda imetabiri ukuaji wa pato la taifa kwa 4% katika mwaka wa fedha 2016/17.

  Takwimu kutoka Ofisi ya Takwimu Uganda zinaonyesha kuwa uchumi ulikua kwa kasi katika nusu ya kwanza ya mwaka huu wa fedha ikilinganishwa na mwaka uliopita.

  Ukuaji wa pato la Taifa katika kipindi hiki ni 7.1% ikilinganishwa na 2.4% katika kipindi sawa na hicho mwaka 2016/17 baada ya kubadilika kwa hali ya hewa na mazao bora ya kilimo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako