• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Somalia na Umoja wa Mataifa watoa wito wa kusimamisha mara moja mapigano kaskazini mwa nchi hiyo

  (GMT+08:00) 2018-05-16 19:47:11

  Rais Mohamed Abdullahi Farmajo wa Somalia na mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Michael Keating wametoa wito wa kusimamisha mara moja mapigano kati ya majeshi ya Somaliland na Puntland baada ya mapigano makali katika eneo la Tukaraq mkoani Sool.

  Katika taarifa yake, rais Farmajo amevitaka vikosi vya Puntland na Somaliland kusimamisha vurugu, hususan wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan. Amesema mapigano hayo yamesababisha vifo na uharibifu wa mali, hayana mantiki na lazima yasimamishwe, na tofauti zote zitatuliwe kwa majadiliano.

  Naye Bw. Keating amezitaka pande zote mbili kufanya majadiliano ya kusimamisha mapigano na kufikia makubaliano ya kisiasa. Amezitaa mamlaka za mikoa hiyo miwili kutafuta suluhisho la amani kwa tofauti zao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako