• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kongamano la kwanza la wanawake la jumuiya ya ushirikiano wa Shanghai lafanyika hapa Beijing

    (GMT+08:00) 2018-05-16 20:50:43

    Kongamano la kwanza la wanawake la jumuiya ya ushirikiano wa Shanghai limefanyika leo hapa Beijing.

    Mada kuu iliyojadiliwa katika kongamano hilo ni kukusanya nguvu ya wanawake na kuhimiza maendeleo ya pamoja. Wajumbe zaidi 200 kutoka nchi wanachama wa jumuiya hilo, nchi wachunguzi, na mashirika ya wanawake walihudhuria mkutano huo na kujadiliana kuhusu wanawake na maendeleo ya uvumbuzi, wanawake na dunia nzuri, na wanawake na ushirikiano wa kunufaishana.

    Naibu spika wa bunge la umma la China ambaye pia ni mwenyekiti wa shirikisho la wanawake la China Bibi Shen Yueyue alihudhuria ufunguzi huo. Katika hotuba yake, Bi Shen ametoa wito wa kuzidisha mawasiliano katika sekta ya wanawake wa jumuiya ya ushirikiano wa Shanghai kwa kupitia kongamano hilo, kuongeza umuhimu wa ushirikiano na mawasiliano ya shirika hilo, kuhimiza manufa ya watu wa nchi wanachama wa shirika hilo, na kutoa nguvu ya wanawake kwa jamii ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako