• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na ujumbe wa chama tawala cha Korea Kaskazini

    (GMT+08:00) 2018-05-16 20:53:47

    Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China leo hapa Beijing amekutana na ujumbe wa Chama tawala cha Wafanyakazi cha Korea Kaskazini unaoongozwa na mjumbe wa ofisi ya siasa ya Kamati Kuu ya chama hicho Park Tae-sung.

    Rais Xi amesema China inaunga mkono Korea Kaskazini kuboresha uhusiano wake na Korea Kusini, kusukuma mbele mazungumzo na Marekani, na kutimiza peninsula ya Korea kutokuwa na silaha za nyukilia. Pia China inaunga mkono Korea Kaskazini kuendeleza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi.

    Bw. Park Tae-sung amesema madhumuni ya ziara yake nchini China ni kutekeleza makubaliano ya pamoja yaliyofikiwa kati ya viongozi wa nchi hizo mbili, na kujifunza uzoefu wa China wa mageuzi na ufunguaji mlango.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako