• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Asilimia 90 ya makubaliano yaliyofikiwa kwenye baraza la ngazi ya juu la ushirikiano wa kimataifa wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" yatekelezwa

  (GMT+08:00) 2018-05-16 21:09:56

  Msemaji wa kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Meng Wei leo hapa Beijing amesema, asilimia 90 ya makubaliano yaliyofikiwa kwenye baraza la ngazi ya juu la ushirikiano wa kimataifa la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" yametekelezwa.

  Amesema pia kuwa, baadhi ya miradi mikubwa, ushirikiano wa biashara na uwekezaji wa uzalishaji, huduma za mambo ya fedha na maingiliano ya utamaduni pia yamepata maendeleo makubwa, na chini ya juhudi za pamoja za pande mbalimbali mwaka mmoja uliopita, kazi husika zimeendelea kwa taratibu na kupata mafanikio. Mkutano wa mwaka jana wa baraza la ngazi ya juu la ushirikiano wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" ulifikia makubaliano ya miradi 279, na mpaka sasa, miradi 255 kati yao imetekelezwa na mingine 24 imeendelea kwa taratibu. Baadhi ya miradi mikubwa kwa mfano reli ya Jakarta-Bandung, ujenzi wa bandari ya Gwadar, na bomba la mafuta kati ya China na Russia imepata maendeleo ya awali. Pia ujenzi wa njia ya Hariri ya Kidijitali ya karne 21 pia umeendelea kwa taratibu, huku safari za treni kati ya China na Ulaya zikizidi 8,000, na kufikia miji 42 ya nchi 14 za Ulaya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako