• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka, Kombe la CAF: Mechi zote mbili za kundi D zaisha kwa sare ya bila kufungana

  (GMT+08:00) 2018-05-17 08:37:01

  Katika mechi za raundi ya pili za hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho la soka barani Afrika zilizopigwa jana, kwenye kundi D lenye timu tatu za Afrika Mashariki matokeo yalikuwa sare kwenye mechi za jana.

  Mjini Dar es Salaam, Wenyeji Young Africans ya Tanzania ilichoshana nguvu na wenzao kutoka Afrika Mashariki Rayon Sport ya Rwanda.

  Lakini Mjini Nairobi, licha ya kuwa kumi uwanjani, wenyeji Gor Mahia waliizamisha sare timu ya USM Algiers ya Algeria.

  Kwa matokeo hayo ya jana, USM inaongoza kwa kuwa na pointi 4, ikifuatiwa na Rayon na Gor amabzo zinafungana pointi, 2 kila moja na Yanga yenye 1 inashika nafasi ya nne na mechi za raundi ya tatu za kundi hilo zitapigwa mwezi Julai baada ya kombe la dunia kumalizika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako