• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka, Kocha wa Al Ahly ya Misri ajiuzulu baada ya timu kufungwa na kwenye mechi dhidi ya KCCA

  (GMT+08:00) 2018-05-17 08:40:21

  Kocha mkuu wa timu ya Al Ahly ya Misri Hossam El Badry amejiuzulu wadhifa wake baada ya timu yake kufungwa kwa magoli 2-0 juzi na KCCA ya Uganda kwenye mechi za raundi ya pili ya hatua ya makundi ya mashindano ya klabu bingwa Afrika.

  Katika barua yake ya kujiuzulu, kocha Badry ameomba radhi kwa uongozi wa timu na mashabiki kwa kile alichosema ni kutotimiza wajibu wake.

  Uongozi wa timu hiyo ulikutana jana kujadili barua hiyo na kukubali uamuzi wa kujiuzulu, na imekabidhi majukumu ya kuifundisha timu hiyo kwa Ahmad Ayoub.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako