• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka, Mashabiki nchini Afrika Kusini wamlazimisha kocha wa Barcelona kumchezesha Messi kwenye mechi ya Kirafiki, Barcelona ilishinda 3-1 dhidi ya Mamelodi

  (GMT+08:00) 2018-05-17 08:41:07

  Kocha mkuu wa Barcelona Ernesto Varvede jana amelazimika kumchezesha Lionel Messi katika mechi ya kirafiki dhidi ya Mamelodi Sundowns ili kukidhi haja ya mashabiki wa soka wa nchini Afrika Kusini.

  Hamu ya mashabiki kumuona Messi akicheza kwenye uwanja wa FNB mjini Johanessburg ilionekana wakati wa mapumziko kocha huyo alipofanya mabadiliko ya wachezaji kumi ambao miongoni mwao hakuwemo Messi, ndipo mashabiki walipopaza sauti wakiita Messi, Messi!

  Lakini baadaye katika dakika ya 74, kocha alifanya mabadiliko na ndipo Messi alipoingia na umati uliokuwepo uwanjani hapo ukaonekana kushangilia kumuona nyota huyo.

  Katika mechi hiyo Barecelona ilishinda kwa magoli 3-1, yaliyofungwa na Luis Suarez, Andre Gomes na Ousmane Dembele na goli la kufutia machozi likifungwa na Sibussiso Vilakazi.

  Mechi hiyo ilikuwa ni maalum kwa ajili ya kuadhimisha miaka 100 ya kuzaliwa kwa baba wa taifa hilo ambaye alikuwa rais wa kwanza wa Afrika Kusini, Nelson Holihlahla Mandela ambaye alifariki mwaka 2013.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako